KUFUATIA  kukamilishwa kwa mechi za duru la kwanza la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kalenda ya soka ya Tanzania sasa inahamia kwenye michuano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), ijulikanayo kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa mechi ya hatua ya 32 Bora katikati ya wiki. 
Vigogo Azam FC na Yanga SC wote wanasafiri kwenda mikoani kumenyana na timu za Ihefu FC na Shupavu FC katika hatua ya 32 Bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC).
Yanga SC wanakwenda Mbeya kuifuata Ihefu, mechi itakayopigwa Uwanja wa Sokoine mjini humo, wakati Azam FC watakwenda Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro kumenyana na Shupavu FC. Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi utahodhi mechi mbili mfululizo za wenyeji, Kariakoo United dhidi ya washindi wa pili wa msimu uliopita, Mbao FC ya Mwanza na Maji Maji Rangers dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro. Green Warriors iliyowatoa mabingwa watetezi, Simba SC itaendelea kucheza nyumbani mjini Dar es Salaam itakapowakaribisha Singida United Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Maji Maji wataikaribisha Ruvu Shooting Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, Njombe Mji FC wataikaribisha Rhino Rangers Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe, Kiluvia United wataikaribisha JKT Oljoro Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani na Ndanda FC watakuwa wenyeji wa Biashara United ya Mara Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Mechi nyingine; Pamba SC wataikaribisha Stand United Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Polisi Tanzania watakuwa wenyeji wa Friends Rangers Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, JKT Tanzania watakuwa wenyeji wa Polisi Dar es Salaam na Mwadui FC wataikaribisha Dodoma FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga. 
Tanzania Prisons wataikaribisha Burkina Faso Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya wakati Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Buseresere FC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. 
Mchezo kati ya KMC ya kocha Freddy Felix Minziro wa Toto Africans ya Mwanza Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam umeahirishwa hadi Februari 7 wakati mechi nyingine zite zinatarajiwa kucheza siku mbili mfululizo, Januari 31 na Februari 1, mwaka huu.
Maji Maji v Ruvu Shooting
Njombe Mji v Rhino Rangers
Kiluvia Utd v JKT Oljoro
Ndanda Fc v Biashara United
Pamba SC v Stand United
Polisi TZ v Friends Rangers
JKT Tanzania v Polisi Dar
KMC V Toto Africans (Imeahirishwa)
Ihefu FC v Yanga SC
Mwadui FC v Dodoma FC 
Green Warriors v Singida United
Tanzania Prisons v Burkina Faso
Kariakoo United v Mbao FC
Maji Maji Rangers Lindi v Mtibwa Sugar
Kagera Sugar v Buseresere FC 
Shupavu FC v Azam F

0 maoni:

Chapisha Maoni