Wadau wa soka Mkoani lindi wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa ILULU  ikiwa ni Michuano ya Fa Cup Tanzania katika hatua ya 32 Bora mkoani Lindi wakati Timu ya Kariakoo Fc itakapovaana na Mbao fc kutoka Jijini Mwanza ili wawatie moyo Wachezaji wa Kariakoo Fc.
 hayo yamesemwa na Peter Msafiri ambaye ni katibu wa Kariakoo akiwa kambini katika maandalizi yao ya Mwisho huku akitaja Viingilio vya mchezo huo kuwa ni sh.2000 .
Aidha kocha wa Kariakoo Abdalah Hassan Malinda amesema Timu aina Majeruhi na wanatarajia Ushindi katika mchezo huo na akisisistiza asilimia 90 ya Wachezaji wa Kariakoo ni watoto kutoka Mkoani Lindi
                           






Mashabiki wa Mbao Fc mkoani Lindi kutoka Kijiwe Cha Boda Boda Saba saba Makaburini  Wameendele Kuiamini Klabu ya Mbao na Kuiombe Ushindi Katika Mchezo wao Utakochezwa Uwanja wa ILULU  ikiwa ni Michuano ya Fa Cup Tanzania katika hatua ya 32 Bora mkoani Lindi wakati Timu ya Kariakoo Fc itakapovaana na Mbao fc kutoka Jijini Mwanza 
Wakizungumza na Mashujaa Fm mashabiki hao ambao ni Rashid Mkilwa na Likambo wamesema Kariakoo Itegemee kufungwa kama inavyotokea kwa Timu kubwa za Ligi kuu Tanzania Bara.

Aidha Mashabiki wa Kariakoo Fc KENETH JONS na Mohammed Suleima(KIGWASU) Wameendelea kuipa Ushindi Timu yao huku wakiseme Kuchezwa cha Mchezo huo Ilulu kunaipa nafasi Kushinda Huku wakiwabeza Mashabiki wa Mbao kutoka mkoani hapa na Kuwataka wawe wazalendo.

0 maoni:

Chapisha Maoni